UTAPIAMLO TATIZO KWA WANANCHI ILEJE

0
584

Na ELIUD NGONDO – ILEJE

WANANCHI wilayani Ileje katika Mkoa wa Songwe, wametakiwa kula chakula kwa afya na si kutuliza njaa ili kuweza kuepukana na tatizo la utapiamlo ambalo limekuwa ni kero kubwa.

Hayo yamezungumzwa jana na Mkuu wa Wilaya, Joseph Mkude katika Kijiji cha Mlale ambako ulifanyika uhamasishaji wa msuala ya lishe kwa
kutumia sanaa, ulioandaliwa na mradi wa kilimo kwa lishe maarufu kwa jina la ATONU.

Mkude alisema wananchi wilayani Ileje wanalima mazao mengi, lakini wameshindwa kupangilia milo yao,  matokeo yake wamekuwa wakila kushibisha matumbo tu na si kwa afya.
Alisema mafunzo yanayotolewa na wataalamu yanatakiwa kuzingatiwa ili kuweza kuiokoa jamii hiyo ambayo imekuwa na asilimia kubwa ya watoto wenye utapiamlo kwa sababu ya kutozingatia ulaji ulio bora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here