24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mkapa aeleza alivyobana fedha hadi akaitwa Mzee Ukapa

Andrew Msechu-Dar es Salaam

RAIS Mstaafu Benjamini Mkapa, ameeleza jinsi wakati wa awamu yake ya kwanza ya uongozi wake alivyobana fedha ili kurudisha uhusiano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF), hadi akapachikwa jina la ‘Mzee Ukapa’.

 Katika kitabu chake cha “My Life, My Purpose” (Maisha Yangu, Kusudio Langu), Mkapa anasema alihakikisha anafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali hasa katika masuala ya uchumi na mahusianio na Benki ya Dunia na Shirkika la Fedha Dunia (IMF).

Anasema kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyokuwepo, alilazimika kuwa karibu naye sana pamoja na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Melkizedeck Sanare na Waziri wa Fedha, Profesa Simon Mbilinyi na Katibu Mkuu wa Hazina, Grey Mgonja.

Anasema alikuwa na mzigo mkubwa katika kujenga uchumi na usimamizi wa mapato na matumizi ya Serikali na anakumbuka Waziri wa Maendeleo ya Nje na Afrika wa Uingereza, Baroness Chalker mwaka 1996, alimweleza kile anachofikiria.

Anasema wakati huo Uingereza ilikuwa ni miongoni mwa washirika muhimu wa maendeleo na ilionyesha kutofurahishwa na namna Tanzania ilivyokuwa ikisimamia fedha za misaada, ambapo Mkapa alimuhakikishia waziri huyo kwamba kutakuwa na mabadiliko na waziri huyo kuhoji ni kwa namna gani ataamini maneno hayo.

Anasema alimjibu kwa kujiamini “unataka nikithibitishie namna gani zaidi ya maneno yangu? Hatuna namna, aidha uamue kuniamini au kutoniamini, lakini utaona tutakapoanza utekelezaji.” 

Anasema anashukuru alimuamini na hatimaye Uingereza ikarejesha misaada yake ya maendeleo kwa Tanzania.

Kwa upande mwingine, anasema Benki ya Dunia na IMF walishasema hawako tayari kutoa ushirikiano iwapo hawataona nia ya dhati ya kuwa na nidhamu katima matumizi ya fedha.

“Niliwaeleza kuwa tutaonesha nidhamu na walitaka uthibitisho, na kwa kuwa katika miezi ya mwanza tulikuwa tukiendesha Serikali kwa kutumia fedha zetu na kila kitu kilisimamiwa vizuri, hatua nilizokuwa nikichukua kufuatilia matumizi ya Serikali hazikuwafurahisha wengi.

“Mamabo yalikuwa magumu na nilianza kulaumiwa kwa kile walichokiita ‘ukapa’ kwa hiyo nikapachikwa jina la utani la ‘Mzee ukapa, ninadhani wale waliokuwa wakinipinga wakati huo kwa sasa wananihurumia. Lakini baada ya muda mfupi, Benki ya Dunia na IMF walilegeza misimamo yao na kurejesha ushirikiano,” anasema.

Anasema alifanya jitihada za dhati za kuhakikisha anarejesha haraka uhusiano mzuri na mashirika hayo ya fedha ya kimataifa na alipata faraja bada ya kupigiwa simu na aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, James Wolfensohn.

“Alinipigia simu akaniamboa, Rais, Hatujawahi kuonana, nadhani unaona watu wetu haoneshi nia ya kuendelea pamoja. Ninakushauri uwaite watu wako uwaeleze kwa kina ugumu uliopo baina ya Serikali yako na Benki ya Dunia. Nami pia nitawapigia na kuwaeleza ugumu uliopo. Iwapo utafanikiwa kuja Washington tutakaa na kuangalia namna ya kuliweka sawa,” anasema.

Anasema baada ya hapo, alijifunza jambo zito kutokana na namna Rais huyo wa Benki ya Dunia alivyompigia simu na kufanya mawasiliano yenye faida, namna alivyokuwa na nia ya kutafuta suluhu, hivyo aliamua kumpigia simu mwakilishi wake nchini, Jim Adams na kufanya mazingumzo, kisha kumpigia aliyekuwa Mkurugenzi wa IMF, Horst Kohler na kuweka vizuri mazingira ya ushirikiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles