24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mkandarasi daraja la JPM atakiwa kukamilisha mradi kwa wakati

Na Clara Matimo, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Jerry Silaa leo Machi 25,2023 imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Daraja la JPM(Kigongo- Busisi) Mkoani Mwanza na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezwaji wa mradi huo.

Akizungumza katika eneo la mradi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi ambao unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Silaa amesema kamati yake imeridhishwa na utekelezwaji wa mradi huo ambao unagharimu Sh Bilioni 716.33 na kufikia asilimia 70 ya utekelezwaji.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ameisisitiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuendelea kusimamia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili daraja hilo likamilike kwa wakati wananchi wawe na uhakika wa kuvuka Ziwa Viktoria kwa urahisi wakitumia dakika nne badala ya Saa mbili wanazotumia sasa.

“Nasisitiza tena daraja hill linajengwa kwa fedha za serikali tunaomba likamilike Februari, 2024 kama ilivyokwenye mkataba, tumekagua mradi huu na mingine ambayo inatekelezwa kwenye mikoa mingine tumepata moyo kwamba nchi hii inajengwa na inafunguka kiuwekezaji.

“Hakika tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hakuna mradi uliosimama na maendeleo yote yanayofanyika yanafanyika katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),”amesema Silaa.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Balozi  Mhandisi Aisha Amour amemtaka mkandarasi anayejenga mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi ambao wameusubiri kwa muda mrefu waanze kuutumia.

“Mradi huu haujawahi kusimama kwa kukosa fedha hivyo namwagiza mkandarasi ahakikishe ifikapo Februari 24, 2024 awe ameukamilisha kwa ubora kama ilivyo kwenye mkataba,tunashukuru sana kamati hii kufika hapa kwenye mradi kuutembelea na kuukagua maana mnawawakilisha wananchi hivyo wakisikia kutoka kwenu watajua kwamba kazi inaendelea,” amesema Mhadisi Amour.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles