28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mkandarasi Badr East Africa arejesha Sh bil 27 alizogushi

Na Upendo Mosha, Moshi

Aliyekuwa Mkandarasi wa Mradi mkubwa wa Maji wa Mwanga, Same na Korogwe, Badr East Africa Enterprises Ltd, ameridhia kurejesha fedha za mradi huo zaidi ya Sh bilioni 27 alizodaiwa kughushi na kujipatia isivyo halali.

Mradi huo ambao inatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya laki nne,alighushi nyaraka hizo na kulipwa malipo ya awali na serikali kinyume na taratibu.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya maji, Mhandisi Antony Sanga, wakati Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo baada ya serikali kusitisha mkataba na mkandarasi huyo.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Waziri wa Maji, Jumaa Awesu, Mhandisi Sanga alisema Mkandarasi huyo alijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu.

Alisema mkataba wake ulisimamishwa ili kuchukua hatua ya fedha hizo kurejeshwa na kuendelea na mradi kwa kupata mkandarasi mwingine.

“Mkandarasi aliyekuwepo alituletea nyaraka feki zilizoghushiwa na kulipwa pesa kiasi cha Sh bilioni 27 ikiwa ni malipo ya awali jitihada za kuzirudisha tulizifanya na tunefanikiwa.

“Kazi iliyokuwepo baada yakusimamisha mradi na kukabidhi mkandarasi huyo kwenye vyombo vya dola alikiri kughushi nyaraka na kujipatia fedha hizo mpaka sasa yupo ndani na sheria unaendelea kufuatwa,” alisema.

Alisema wafadhili waliokuwa wakifadhili mradi huo waligoma kuendelea kutoa fedha za kuendelea na ujenzi kwa masharti ya fedha za awali zilizolipwa kwa wakandarasi zirejeshwe ili waweze kuendelea jambo ambalo serikali ipo tayari na italipa bilioni mbili.

Akizungumza na viongozi hao,Waziri Aweso, alisema mkandarasi huyo amekubali kurejesha kiasi hicho cha fedha ambapo utekelezaji wa mradi ambapo aliwatakana wataalamu wa maji kuacha tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi kwa maslai binafsi.

“Kwa sasa fedha zinarudishwa lakini nawaomba wataalamu muache tabia ya kuongeza gharama kwenye miradi ya maji fedha hizi ni za wananchi hatuwatendei haki lakini pia miradi ya maji sio ya wizara viongozi wote mnahaki ya kuitembelea maana nataka uwazi,” alisema Aweso.

Aidha alisema serikali imetenga zaidi ya Bilioni 19 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji mkoa wa Kilimanjaro ambapo mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (MUWSA) imetengewa Sh bilioni 6.7 na Sh bilioni 12.3 kwaajili ya halmashauri zote.

Mbunge wa jimbo la Mwanga (CCM), Joseph Thadayo amewataka wataalamu kusimamia miradi hiyo kikamilifu ili kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles