28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Tanzania kuondoka na Mercedes Benz mpya

Na Jeremia Herenest, Mtanzania Digital

WALIMWENDE 20 kutoka Kanda Nane nchini wanatarajiwa kuchuana kuwania taji la Miss Tanzania, Mei 20, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mshindi ataondoka na gari jipya aina ya Mercedes-Benz.

Mapema Mwezi huu Warembo hao waliingia kambini kwa ajili ya kupewa mafunzo mbalimbali pamoja na kushiriki mataji madogo madogo ambayo yatatolewa siku ya fainali.

Akizungumza Dar es Salaam leo Mei 18, Afisa Masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa, amesema mwaka huu watatoa zawadi mbalimbali ikiwamo gari hilo aina ya Mercedes Benz.

“Mwaka huu tumezidi kuheshimisha shindano hilo kwa kutoa zawadi kubwa ambayo haijawahi kutolewa ni gari yenye thamani ya milioni 40 aina ya Mercedes Benz ziro kilometa,” amesema Malisa.

Ameongeza kuwa mshindi wa tano atapewa zawadi ya Sh milioni 1, wanne milioni 1, watatu milioni 3 na mshindi wa pili milion 5 na zawdi nyingine zitatangazwa siku ya fainali.

Mbali ya mchuano huo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wabongo fleva akiwamo, Ben Poul, Barnaba na Bendi. Kuhusu viingilio amesema kuna Sh 50,000 kawaida, VIP 100,000, VVIP 200,000, 130,0000 kwa VIP meza ya watu kumi na 180,0000 kwa VVIP meza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles