Miradi ya maji Chalinze kukamilika mwakani

0
501

Na Mwandishi Wetu, Pwani

MENEJA wa Dawasa-Chalinze, Onest Makoi, amesema miradi yote ya maji inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2021 na amewataka wananchi wawe tayari kwa maboresho hayo ikiwamo upanuzi wa miundombinu ya maji, umaliziaji wa ujenzi wa matenki na usambazaji wa maji awamu ya tatu.

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete (kulia), akizungumza na Meneja wa Dawasa-Chalinze, Onest Makoi (wa pili kulia) na watendaji wengine wa Dawasa baada ya jana kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa katika jimbo hilo. Na Mpigapicha Wetu.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati wa ziara ya Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete ya kutembelea miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa jimboni humo.

Pia amesema ujenzi wa Mradi wa Ruvu-Mboga uko katika hatua ya mwisho kwa kuwa ununuzi wa vifaa vya ujenzi unatarajiwa kukamilika.

Baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya miradi hiyo na kuongea na watendaji wa Dawasa, Ridhiwani, amewashukuru Dawasa kwa hatua kubwa wanazoendelea kufanya na kumshukuru, Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaangalia wananchi wanyonge wa Chalinze kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali ikiwamo za maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here