‘Grateful’ ya Julien Rashidi yatua Bongo

0
639

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KUTOKA Perth, Western Australia mwimbaji nyota wa Injili, Julien Rashidi, amewashukuru wapenzi wa muziki huo kwa mapokezi makubwa ya wimbo wake, Grateful alioachia hivi karibuni.

Julien mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameliambia MTANZANIA kuwa amepata mrejesho mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Afrika Mashariki hasa Tanzania ikiwa ni pamoja na wimbo Grateful kuingia kwenye chati mbalimbali za muziki.

“Kila mtu anajua Mungu kule ambako amemtoa hivyo ni vizuri kumshukuru ndio maana kupitia wimbo, Grateful nimepokea shuhuda nyingi za watu walioguswa na ujumbe huu. Video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, Apple Music na Spotify,” alisema kiongozi huyo wa huduma ya NGIC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here