It all about Cards wajitosa kudhamini Miss Tanzania

0
530

NA JEREMIA ERNEST

Mdhamini wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2020, Amina Swedi kutoka Kampuni ya (it’s all about cards) ambayo inajihusisha na kutengeneza kadi za shughuli mbalimbali amesema amejitosa kudhamini shindano hilo kwa sababu lina ibua viaji vya wanawake.

Akizungumza na MTANZANIA Digital leo Ijumaa, Novemba 27, Amina amesema wasichana wengi wanafanya vizuri katika tasnia za sanaa pamoja na kusaidia jamii wametoa katika shindano hilo.

“Mchango wa shindano la Miss Tanzania katika Serikali na jamii ni mkubwa hata katika utendaji kazi wao, mfano mzuri ni Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Joketi Mwegelo na wengi ambao wameanzisha taasisi mbalimbali za kusaidia jamii,” amesema Amina.

Ameongeza kuwa udhamini wake mwaka huu umehusika katika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo mataji ya warembo watakayo vishwa katika fainali hizo.

Hata hivyo, Amina pia amesema kwa mwaka huu anategemea kuona Mshindi ambae ni mrembo na mwenye ufahamu mzuri atakaye piga hatua ya mbele zaidi katika fani hiyo.

Kampuni ya it’s all about cards imekua ikidhamini mashindano hayo ya urembo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo tangu yaanze kuratibiwa na Kampuni ya The Look Campony Limited.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here