25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Milipuko Marekani haihusiani na ugaidi wa kimataifa

andrew-cuomoNEW YORK, MAREKANI

GAVANA wa New York Andrew Cuomo amesema mripuko uliotingisha wilaya ya Manhattan mjini hapa Jumamosi iliyopita na kujeruhi watu 29 hauonekani kuhusiana na ugaidi wa kimataifa.

Aliapa kwamba wahusika watasakwa na kushtakiwa na kwamba polisi wa ziada 1,000 wamewekwa huko Chelsea, kitongoji cha wakazi upande wa magharibi wa Manhattan ambao unajulikana kwa maduka mengi ya sanaa na kuna na idadi kubwa ya mashoga.

Gavana huyo amewataka wakazi wa New York waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Gavana huyo wa chama cha Demokrat amesema uchunguzi wa awali hauonyeshi kuwepo na uhusiano na ugaidi wa kimataifa na kuwa hakuna kundi la kigaidi lililodai kuhusika.

Aidha maafisa wa serikali wanasema mripuko huo wa Manhattan hauonekani kuwa na uhusiano na mripuko wa bomba ulitokea mapema Jumamosi huko New Jersey na kulazimisha kufutwa kwa mbio za hisani.

Afisa mmoja wa polisi ameliambia Shirika la Habari la AP kuwa kifaa cha pili ambacho maafisa wamekichunguza kutoka majengo manne eneo la tukio kinaonekana kuwa cha kuivisha chakula na kiliunganishwa na waya na simu ya mkononi.

Afisa huyo ambaye hakutaja jina lake litajwe kwa kuwa haruhusiwi kuzungumzia uchunguzi unaoendelea amesema kifaa hicho kimepatikana ndani ya mkoba wa plastiki katika Mtaa wa 27 Magharibi.

Kifaa hicho kiliondolewa kwa kutumia roboti na kupelekwa idara ya zima moto kwa uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles