30.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Makubaliano ya kusitisha mapigano yamalizika Syria

syriaDAMASCUS, SYRIA

MAKUBALIANO ya siku saba ya kusitisha mapigano yaliyotangazwa na Jeshi la Syria yamemalizika usiku wa kuamkia jana huku kukiwa hakuna taarifa ya haraka ya kuyarefusha.

Makubaliano hayo yaliyoandaliwa na Urusi na Marekani yalianza kutekelezwa tangu Jumatatu iliyopita ingawa pande zote mbili za waasi na serikali zimekuwa zikitupiana lawama kwa uvunjaji wa makubaliano hayo.

Muungano wa majeshi yanayoungwa mkono na Marekani ulifanya mashambulizi na kuwaua askari kadhaa wa serikali mwishoni mwa wiki mjini Aleppo, kitendo ambacho Marekani imeeleza kukijutia ikisema ilidhani ni wanamgambo wajiitao Dola la Kiislamu (IS).

Lengo kubwa la makubaliano hayo ilikuwa ni kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wananchi walionaswa uwanja wa mapambano.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa (UN) umesema misaada iliyokuwa imekwama mpakani mwa Uturuki na Syria kwa wiki nzima ilikuwa bado haijafikia maeneo yaliyozingirwa mashariki mwa Aleppo.

Watu karibu 270,000 waliokwama bado hawana huduma ya maji, chakula, malazi na matibabu mjini Aleppo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,464FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles