24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mila potofu zikiwekwa pembeni zitasaidia wanawake

Janeth Mushi -Arumeru

BAADHI ya mila na desturi potofu miongoni mwa jamii zikiwekwa pembeni zitachangia ongezeko la wanawake na vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Kauli hiyo, iliyotolewa juzi na mmoja wa wakazi wa eneo la Ngaramtoni wilayani hapa mkoani Arusha, Edwin Johnson akizungumza wakati wa ‘road show’ ya uhamasishaji wa wanawake na vijana kuwania nafasi za uongozi.

Kupitia mradi wa kukuza ushiriki wa wanawake na vijana kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi za 2019/20 (Wypre), unaoadhifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) na kutekelezwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla),tawi la Arusha, uhamasishaji huo ulifanyika kata za Olmotony na Olorein.

Alisema elimu kwa jamii ni muhimu kutolewa ili kupunguza na kumaliza baahdi ya mila na desturi zinazochangia wanawake kushindwa kuwania nafasi za uongozi.

“Uhamasishaji huu, utasaidia wanawake kuwa wajasiri na watajitokeza kwa wingi tukianzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, itakuwa fursa nzuri kwao.

“Baadhi ya mila na desturi mbaya zinaathiri sana maendeleo ya kina namna,suala la uongozi  mila na desturi zikiwekwa pembemi kila mtu atakua na imani juu ya mwenzake kila mtu atamheshimu mwenzake hasa utu,utu ukiheshimika kila mtu atatumia kipawa chake,”alisema.

Mwanasheria wa chama hicho,Ekael Michael, alisema lengo la mradi ni kuongeza idadi ya ushiriki wa makundi katika chaguzi zinazokuja.

Naye Tumaini Naimani alisema elimu  itasaidia  wanawake kupata wawakilishi katika ngazi za maamuzi na kuwa elimu zaidi ya uhamasishaji inapaswa kutolewa hasa kwa maeneo ya pembezoni.

“Ni vema kutangaza kutuhamasisha wanawake kugombea, tukiwa na wawakilishi itasaidia tutahehsimima katika jamii nzima na wamama watapata fursa kusema matatizo yao kwa kiongozi,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles