30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Elimu ya sheria yapunguza mauaji ya vikongwe

Ramadhan Hassan -Dodoma

UTOAJI wa elimu unaofanywa na wasaidizi wa kisheria  maeneo ya kanda ya ziwa, kumetajwa ndiyo sababu ya kupungua mauaji ya vikongwe.

Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na mwakilishi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la  Kasodeko, Marius Isavika  wakati wa ufungaji wa  mafunzo rejea ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria Tanzania kwa wasaidizi wa kisheria nchini.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la LSF.

Alisema kupitia mradi wa kuimarisha upatikanaji wa haki kisheria, wameweza kutoa elimu  maeneo ya kanda ya ziwa kuhusu na madhara ya mauaji kwa vikongwe.

“Moja kati ya jambo ambalo tunajivunia ni kupungua mauaji kanda ya ziwa, sisi tunatoka Simiyu, sababu ni elimu ambayo tumeitoa…sasa hivi hakuna tena mauaji,” alisema.

Alisema changamoto wanayokutana nayo wasaidizi wa kisheria, ni kuwa wachache hivyo kutokuwafikia watu wengi na kwa wakati.

“Kukabiliana na changamoto hii,tumekuja na mobile kliniki ambazo zinatembea maeneo ya vijijini na kuwafikia watu wengi,”alisema.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng’wanakilala alisema mafunzo hayo ya siku tano yalikuwa kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali, ikiwemo jinsi ruzuku wanazotoa zinavyowanufaisha wananchi.

“Tumekuwa hapa kuangalia jinsi gani ruzuku tunazotoa zinawasaidia watu wenye matatizo, walengwa wanafikiwa,”alisema.

Alisema kuna maeneo kina  mama wanateseka sababu ya kukosa msaada wa kisheria hususan katika masuala ya migogoro ya ardhi na ndoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles