21.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Migororo ya ardhi yazidi kufukuta Pwani

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

SIKU chache baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo kushughulika na wavamizi na matapeli wa viwanja wilayani Bagamoyo, uvamizi umezidi kushika kasi.

Itakumbukwa Desemba 5, mwaka huu, akiwa mkoani Pwani kwenye kikao maalumu cha Serikali na wawekezaji, Waziri Lukuvi alisema mkoa huo unaongoza kwa kuwa na wavamizi na matapeli wa ardhi na kumuagiza Mhandisi Ndikilo kuchukua hatua kali, huku akiahidi kusuka safu mpya wa watendaji.

“Kuna watu mkuu wa mkoa kwa takwimu za leo mkoa wa Pwani ndiyo unaongoza kwa matapeli na wavamizi wa ardhi, kuna watu wanamiliki ardhi zao kisheria, watu wananoa visu vyao na mapanga Dar es Salaam wanaishi kwenda kufukuza watu kwenye maeneo yao, sasa naomba hili unisaidie,” alisema Lukuvi.

Pamoja na tamko hilo, linaokena halijawashtua wavamizi hao, kwani ndiyo kwanza kumekucha kwani vitendo hivyo viko palepale kwa watu wanaomiliki maeneo yao kuonewa.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, mmoja wa wananchi wanaokumbana na kadhia hiyo, Sharifa Sabeho alisema kumekuwa na mchezo mchafu unaonendelea kwenye eneo lake la hekari 18 eneo la Mapinga wilayani humo ambalo kwa nyakati tofauti kumekuwa na kundi la watu ambao wamekuwa wakivamia eneo hilo nakuanza kupima huku wakitoa vitisho.

 “Mimi nina eneo langu la hekari 18 ambalo nalimiliki kisheria tangu 2004, jambo la kushangaza ni kwamba kumekuwa na watu ambao wamekuwa akifika kupima eneo langu kwa madai kuwa ni lao ilihali  mimi nalimiliki kisheria na hati ninazo,” alisema Sharifa.

Alisema amekuwa mtu wa kuzunguka kila siku kuhakikisha eneo lake linakuwa salama jambo ambalo linamnyima fursa ya kufanya kazi za ujenzi wa taifa kama Rais Dk. John Magufulia anavyosisitiza.

“Ombi langu mimi ni kwa Waziri Lukuvi na jeshi la polisi kwani naamini kuwa ndio wanaweza kunisaidia kutokana na uvamizi huu ninaofanyiwa mara kwa mara bila msaada,” alisema Sharifa.

Kauli ya Lukuvi

Mbali na waziri Lukuvi kutoa maagizo kwa mkuu wa mkoa,aliahidi kuongeza nguvu ikiwamo kuweka watendaji wapya na kanda maalumu ya kusimamia mkoa huo.

“Naamini tutashirikiana, watu wengi sana wanadhurumiwa ardhi zao hapa Kibaha,Bagamoyo kwa tishio la silaha za jadi wanaongoza.

“Sasa nafikiri kwamba moja ya tatizo pengine labda hakuna wataalamu wazuri wa mipango miji, hilo nitawasaidia, Januari,mwakani, nitafanya uteuzi upya kuanzia kamishna maalumu wa kusimamia ardhi na mkurugenzi msaidizi wa upimaji wa ramani,” alisema Lukuvi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles