23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yawataka wananchi kufanya mabadiliko Kawe

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM 

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Lucy Malongo,  amewataka wakazi wa jimbo la Kawe wajiandae kufanya mabadiliko ya kiuongozi kwani mwakilishi waliyemchagua  ameshindwa kuwatumikia sawasawa.

Akitoa madai hayo amesema Mdee ameshindwa kuwajibika hvyo n vema wafanye mabdiliko katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Kauli hiyo aliitoa jana, alipokuwa akiwatambulisha viongozi wapya wa Serikali za Mitaa  katika mkutano uliofanyika Mtaa wa Dovya Kata ya Bunju, ambapo Lucy alidai mbunge huyo hayuko makini katika utumishi wa wananchi na sasa wanatakiwa kumuondoa.

“Kama tunavyofahamu mwakani tunaingia kwenye uchaguzi mkuu ujao katika jimbo lenu hakuna mwakilishi makini, hivyo jiandaeni kupata mbunge mchapa kazi atakayekuwa na muda wa kutosha kutumikia wananchi wake,” alisema Lucy.

Alisema kuwepo kwa viongozi wanaotokana na CCM madarakani kama wenyeviti na wajumbe ni fursa kwa chama hicho na wasidhani kuwa Chama hakiwahusu bali waongeze jitihada kuhakikisha uchaguzi ujao kinashinda nafasi zote.

Lucy aliwataka viongozi kuacha tabia ya kuwatoza fedha wananchi wanapofika ofisini kwa ajili ya kupata huduma  badala yake wajipange kuangalia namna ya kuleta maendeleo na kuungana na kasi ya rais katika utekelezaji wa ilani ya chama.

Alisema mwenyekiti na wajumbe wake kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha mtaa wao unakuwa salama.

“Mwenyekiti mpya hakikisha unatatua migogoro na kero za wananchi kwa wakati sambamba na kuachana na rushwa badala yake wafanye kazi ka kusimamia taratibu ili kuleta maendeleo,” alisma Lucy.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dovya, Razalous Mwakiposa aliwataka wakazi wa mtaa huo  kushirikiana nao kukomesha uchimbaji wa madini ya mchanga unaofanywa bila kuzingatia taratibu ili kuzuia mmomonyoko wa adhi unaoweza kuleta maafa kwa wakazi. 

“Mbali na kukabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara pia inakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wachimbaji wa madini ya mchanga pasipo kufuata taratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles