33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lipumba ataja machungu ya mwaka 2019

NA LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibraim Lipumba ametaja machungu ambayo taifa na chama chake kimepitia katika kipindi cha mwaka mzima wa 2019.

Akizungumza na waaandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na chama hucho kufiwa na mwenyekiti wa kwanza wa CUF, marehemu James Mapalala na ajali ya lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Kuhusu khali ya uchumi alisema Watanzania wengi hali imekuwa ngumu ambapo taarifa ya furaha duniani ya mwaka huu, ilionesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne kati ya nchi 156 kwa watu wake kutokuwa na furaha ikitanguliwa na Afganstan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini ambazo zote zinakabiliwa na matatizo ya kisiasa na vita ikishuka kutoka nafasi ya nane mwaka 2012.

Profesa Lipumba alisema licha ya takwimu za Serikali kuonesha asilimia ya umasikini imepungua kutoka 34.4 mwaka 2007 hadi 26.4 mwaka 2018 kwa kutumia kigezo cha mtu mzima kutumia Sh 50,000 kwa mwezi, lakini ikiwa watatumia kigezo cha kimataifa cha Dola 1.90 karibu nusu ya Watanzania wako katika lindi la umaskini.

“Ili Tanzania itokomeze umaskini ni muhimu kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo. Wakulima wengi wa korosho wameathirika na sera za Serikali zilivyotekelewa katika ununuzi wa korosho.

“Hawajalipwa fedha zao na msimu wa 2017/2018. Pia kuna wakulima wa pamba ambao hawajaliwa fedha za msimu uliopita.

“Takwimu za Serikali zinaonesha uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.1 mwaka 2018,wataalamu wa Benki ya Dunia wanakadiria ukuaji halisi wa uchumi ni asilimia 5.4,,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema  mazingira ya kufanya biashara yameendelea kuwa magumu, utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia kuhusu wepesi wa kufanya biashara mwaka 2019, unaonesha Tanzania ni ya 141 kati ya nchi 190.

Alisema  ugumu wa kufanya biashara umesababisha kupungua kampuni mpya zilizosajiriwa kutoka 8,890 mwaka 2015 hadi 5,276 mwaka jana, ikilinganishwa na Rwanda ambayo ziliongezeka kutoka 9,775 hadi 1,0635 katika kipindi kama hicho.

Kuhusu hali ya siasa, alisema Tanzania imerudi nyuma katika ujenzi wa demokrasia kutokana na sintofahamu iliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba, mwaka huu, baada ya vyama vya upinza  kususia uchaguzi,huku wagombea wao kunyimwa fursa ya kushiriki.

“Kimsingi uchaguzi wa Serikali za mtaa haukufanyika, zaidi ya asilimia 90 ya wagombea wa CUF waliojitikeza kugombea uongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa hawakupewa fursa ya kugombea. Kwa kunyimwa fursa za kugombea au kuenguliwa baada kujaza fomu ya kugombea, tulilazimika kutoshiriki uchaguzi huo baada ya wagombea wetu kuondolewa.

“Taasisi iliyofuatilia maendeleo ya demokrasia na uhuru duniani (Fredom House) katika taarifa yake ya mwaka 2009, Tanzania imepata alama 45 kati 100 ukilinganisha na alama 52 mwaka 2018,alama 58 mwaka 2017, alama 60 mwaka 2016, alama 63 mwaka 2015, utafiti huu unaonyesha hali ya uhuru na Demokrasia imekuwa inapungua mfululizo katika kipindi cha awamu ya tano,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema ni muhumu Rais kutambua ujenzi wa demokrasia ni sehemu ya maendeleo hivyo kuwanyima wananchi fursa ya kugombea na kuchagua viongozi wanaowataka ni kudumaza maendeleo ya kisiasa na kijamii.

Profesa Lipumba alisema kuwa amani ya kweli ya nchi itaathirika ikiwa yaliofanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa na chaguzi za marudio yataendelezwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwakan.

Profesa Lipumba alimwomba rais kuwaachia masheikh mbalimbali, akiwamo Msellem, Farid na wenzao ili waweze kuungana na familia zao kama alivyowasamehe wafungwa 5,533 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, huku akieleza kusikitishwa na idadi kubwa ya mahabusu wapatao 18,256.

Alisema  chama hicho, kitasimamisha wagombea ngazi zote za katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles