WAFUGAJI mkoani Geita wamehimizwa kujitokeza kupiga chapa mifugo yao kwa kuwa hatua hiyo inasaidia kudhibiti wizi wa mifugo na kuwafanya kuitambulika haraka, anaripoti Harrieth Mandari.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema pamoja na idadi kubwa ya wafugaji kujitokeza, bado viongozi na watendaji wanapaswa kuendelea kuwahimiza wafugaji waliosalia kujitokeza na kupiga chapa ng’ombe wao.
Alisema upigaji chapa ni agizo la Waziri Mkuu aliyetaka ng’ombe wote nchini wapigwe chapa kuondokana na tatizo la wimbi la wizi wa mifugo na pia kusaidia kujua takwimu kamili za ng’ombe nchini.