MBUNGE wa Serengeti, Marwa Ryoba, ameutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari Serengeti kumpangia vipindi aweze kufundisha wanafunzi wa shule hiyo masomo ya sayansi anapokuwa mapumziko, anaripoti Malima Lubasha.
Ryoba alisema hayo wakati wa makabidhiano wa msaada wa madawati na magodoro yaliyotolewa na kampuni inayojishughulisha na utalii ya Grumeti Reserves Fund.
Alisema amechukua hatua hiyo baada ya kuridhishwa na matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka huu ambako wanafunzi wote 48 wamefaulu, daraja la kwanza wakiwa 12, daraja la pili 34 na la tatu wamefaulu watatu.