25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YATAIFISHA VIWANDA 10

Serikali imetaifisha viwanda 10 mara baada ya kubainika kuwa wamiliki wake walivunja makubaliano baada ya mikataba ya mauzo kuchambuliwa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alivitaja viwanda hivyo ni pamoja na  Korosho Lindi, Mgodi wa Pugu Kaolin, Kiwanda cha Mkata Saw Mills Ltd, Manawa Ginnery Co.Ltd, Dabada Tea, Tembo Chipboard Ltd, Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills,  Mang’ula Mechanical and Machine Tools Co. Ltd, National Seal Co-operation na Porikasadar, huku mmiliki wa Kiwanda cha Mwanza Tanneries kikirudishwa serikalini na mmiliki kwa ridhaa yake mwenyewe.

“Msajili wa Hazina haelewi kwanini rais alikuwa anasema futa hii ina maana viwanda vyote vina hati na hati zote hutolewa na Serikali hivyo viwanda hivi tunavirudisha kwetu.

“Orodha hii si ya mwisho, wataalamu wapo kazini tunataka zoezi hili tulimalize Agosti 22 kama hadi siku hiyo kuna mtu hajafika ofisini basi itakuwa ni bahati mbaya kwani tungependa viwanda vyote vifanye kazi, wawekezaji wa viwanda hivi tunawataka kulinda viwanda vyao hadi makabidhiano rasmi na Ofisi ya Msajili Hazina yatakapofanyika,” amesema.

Aidha, amesema viwanda ambavyo serikali itavichukulia hatua kuwa ni Sabuni Industries Ltd, Tanzania Moshi Pesticides, Tanzania Bag Corporation, Ilemela Fish Processing Plant na Mzizima Maize Mill huku na kuongeza kuwa viwanda vilivyobadilisha matumizi bila idhini ya Msajili wa Hazina, bila kujali kama wanazalisha bidhaa na kutoa ajira wanatakiwa kuwasiliana na Msajili wa Hazina haraka iwezekanavyo.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles