25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mganda afichua siri ya usajili Yanga

NA MWAMVITA MTANDA-DAR  ES SALAAM

MSHAMBULI  mpya wa Yanga, Mganda,  Juma Balinya, amefichua kuwa, kabla ya kumwaga wino wake kwa Wanajangwani hao,  alikuwa ofa kutoka klabu tatu.

Balinya ambaye ni kinara wa mabao wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya nchini Uganda, akipachika mabao 19, akiwa na timu ya Polisi, juzi alitambulishwa rasmi kuwa mchezaji  mpya wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Utambulisho wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ulifanyika wakati wa harambee ya uchangiaji  ya klabu ya Yanga iliyopewa jina la ‘Kubwa Kuliko’ iliyofanyika juzi Ukumbi wa Diamond  Jubilee jijini Dar es Salaam.

Balinya ni miongoni mwa wachezaji nane wa kimataifa,  ambao  tayari wamemwaga wino wa kuichezea  Yanga, msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Balinya alisema alihitaji zaidi kucheza soka nchini kwao Uganda, lakini ushawishi wa Yanga ulimfanya kubadili nia yake ya awali.

“ Mimi ni mchezaji ambaye natambua uwezo wangu, timu nyingi zilinihitaji mara tu  msimu  ulipomalizika, lakini Yanga walionekana kuwa na umuhimu zaidi na mimi, ndio maana walivyotuma tiketi nikaja haraka kumalizana nao.

“Nilikaribia kujiunga na Horoya ya Guinea, lakini wiki mbili baada ya kutumiwa ujumbe, nikaona posti za Heritier Makambo ambaye pia akikuwa mchezaji wa Yanga tayari amesaini.

“Kiukweli Yanga walinisaka kwa hali na mali  na waliponipata walinieleza kuwa  wanahitaji mchezaji wa aina yangu, ili nizibe pengo la Makambo,”alisema Balinya.

Alisema, hakuwa na sababu kubwa ya kuumia, baada ya kuikosa Horoya kwa anaamini anao uwezo mkubwa wa kucheza timu yoyote na kupata mafanikio.

“Yanga wasiwe na wasiwasi , wamepata mtu mpambanaji, nitapambana kuhakikisha naisadia kufanya vizuri katika Ligi Kuu na michuano ya kimat aifa,”alisema.

Balinya alisema, anao uzoefu mkubwa wa kushiriki michuano ya kimataifa, hivyo ana imani atakabilina na kibarua cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akibainisha kuwa, baadhi ya timu zitakazopigania kinyang’anyiro hicho amewahi kuzichezea hivyo anafahamu undani wao.

“ Mchezaji hatakiwi kuwa na uonga,  sababu kuna wakati unaweza kukutana na timu ngumu lakini lazima upambane, na ukiamua kufanya jambo hakikisha  litafanikiwa,”alisema.

Alisema, anatambua ubora wa Makambo ambaye amemuachia nafasi hiyo, hivyo atajitahidi kufanya vizuri zaidi ili asiwaangushe waajiri wake ambao wamemuamini na kumpa mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Straika huyo aliwaomba wadau na mashabiki wa Yanga

nchini, wampokee kwa mikono miwili ili kumpa mzuka wa kufanya kile kilichomleta Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles