24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

EXIM yapewa tuzo uchangiaji damu

Na MWANDISHI WETU -MWANZA

BENKI ya Exim Tanzania imekabidhiwa tuzo maalumu kutoka serikalini, ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha upatikanaji wa damu salama.

Exim imekabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa maadhimisho ya uchangiaji damu yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza wiki iliyopita.

Waziri Ummy aliihimiza benki hiyo kuendelea kuwa balozi imara wa damu salama nchini na kuhamasisha taasisi nyingine na watu binafsi kuungana na benki hiyo kufanikisha mpango huo.

“Serikali imetenga Sh bilioni 5 mwaka wa fedha 2019/20, zitakazotumika kujenga vituo vidogo vya uchangiaji damu salama katika mikoa 12 nchini,” alisema.

Katika maadhimisho hayo, Ummy pia alizindua mashine mpya ‘full automation’ za kupima maambukizi katika damu na za kupima makundi  ya damu ambazo zimesimikwa kwenye vituo vya kanda sita vya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya.

“Tunataka kumfikia kila Mtanzania mwenye mahitaji ya damu salama popote alipo, tuhakikishe anapata damu salama bila kikwazo chochote. 

“WHO inakadiria idadi ya watu 1,000 zipatikane chupa 10 za damu, Watanzania tunakadiriwa tupo milioni 55, tunapaswa kupata asilimia moja ya idadi hiyo, hivyo chupa 550,000 zinahitajika kila mwaka kutosheleza mahitaji,” alisema.

Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Exim, Stanley Kafu alisema wamepokea tuzo na heshima hiyo kutoka serikalini kwa mikono miwili  kwa kuwa ni sehemu ya matokeo chanya ya mkakati wao wa uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles