23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Maurizio Sarri aondoka Chelsea

LONDON, ENGLAND 

UONGOZI wa timu ya Chelsea, umethibitisha kuwa, kocha wao Maurizio Sarri ameondoka baada ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja na sasa amejiunga na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus.

Kocha huyo amefikia makubaliano ya kujiunga na Juventus kwa mkataba wa miaka mitatu ambao utakuwa na thamani ya pauni milioni 18 kwa kipindi hicho chote.

Kwa sasa Chelsea wapo kwenye mipango ya kumtangaza kocha mpya ambaye atakuja kuchukua mikoba ya kocha huyo, hivyo jina la nyota wa zamani wa timu hiyo Frank Lampard ambaye kwa sasa ni kocha wa Derby, linatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wanawaniwa.

Sarri bado alikuwa na mkataba wa miaka mwili mbele, lakini ameondoka kutokana na mashabiki kuto furahia falsafa za kocha huyo kwa wachezaji wake.

Kutokana na hali hiyo, wamekubali kutoa pauni milioni 7 kama sehemu ya kufidia kuvunja kwa mkataba wake na sasa anakwenda kuchukua nafasi ya kocha Massimiliano Allegri ambaye ameondoka katika kikosi hicho cha mabingwa.

Kwa sasa Sarri atakuwa anachukua kitita cha pauni milioni 6.2 kwa mwaka ndani ya Juventus. Hata hivyo kocha huyo alikuwa na furaha kurudi nchini Italia kwa ajili ya kwenda kukaa karibu na familia yake.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Sun la nchini Uingereza, uongozi wa Chelsea bado ulikuwa na mpango wa kuendelea kuwa na kocha huyo kwa ajili ya msimu ujao, ila kocha mwenyewe alikwenda kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa timu hiyo Marina Granovskaia na kumwambia kuwa anataka kuondoka.

“Nilifanya mazungumzo na Sarri mara baada ya kumalizika kwa fainali ya Kombe la Europa na aliweka wazi kuwa anataka kuondoka na kurudi Italia kwa ajili ya kuwa karibu na familia yake, hata hivyo tunashukuru kwa kile alichokifanya kwetu kwa kipindi chote hasa kwa kuchukua ubingwa wa Europa na kuifanya timu imalize nafasi ya tatu kwenye Ligi, tunamtakia kila la heri,” alisema Marina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles