29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MFUMO MPYA WA KUNUNUA LUKU, BILI ZA MAJI, TRA, FAINI ZA TRAFKI WAFAFANULIWA

 

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


KUANZIA Aprili mosi mwaka huu taasisi zote za Serikali zitafanya malipo kwa mfumo wa kielekroniki kupitia Wakala wa Tehama wa Serikali (E-government) na si kampuni binafsi ikiwema Maxmalipo, imefahamika.

Taarifa kutoka serikalini kupitia mfumo huo upo chini ya Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government  Agency), ambayo uliweka mkakati hadi kufikia Juni mwaka huu taasisi na idara zote za Serikali zifanye malipo kwa kutumia mfumo huo.

Kutokana na maelekezo hayo hadi sasa tayari taasisi zinazotumia mfumo huo ni Mamlaka ya Mapato (TRA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Jeshi la Polisi na Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka (Dawasa).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo taasisi hizo zilishaanza kufanya malipo kwa majaribio na kwamba zimefanya vizuri na hivyo kuingia moja kwa moja katika mfumo huo.

Taarifa kutoka ndani ya taasisi ya Wakala ya Serikali Mtandao Mtandao (e-Government  Agency), zimeeleza kuwa wao kutengenezwa kwa mfumo huo ulikuwa mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita.

Chanzo hicho cha habari kinaeleza kuwa baada ya kuelekeza mpango huo kwa serikali Wizara ya Fedha ndiyo watakaokuwa wasimamizi wakuu.

Baadhi ya mashirika yameshaanza kutangaza huduma hizo kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo nalo litajiunga Aprili 1, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Leila Muhaji, wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) wataunganishwa Aprili 2 .

“Kuanzia Aprili 2, mwaka huu Tanesco itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

“TANESCO ikiwa miongoni mwa taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki,’’ alieleza Leila katika taarifa hiyo.

“Pia Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa shirika hilo la umeme watahakikisha mfumo huo unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU,” alisema.

Hadi sasa taasisi nyingine za Serikali ambazo zimeanza kutumia mfumo huo kwa mafanikio ni Polisi, Brella, Wizara ya Ardhi, TRA pamoja Dawasco.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles