31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WALIOTAKA MWIGILU, NDALICHAKO WAJIUZULU YAWARUDI

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WANAFUNZI sita wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamepewa barua za onyo kwa kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria.

Wanadaiwa kuhamasisha maandamano ya kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba ajiuzulu kutokana na kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), marehemu Akwilina Akwilini, aliyeuawa kwa risasi Februari 16, mwaka huu.

Barua hizo zilizosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Profesa David Mfinanga, kwenda kwa wanafunzi hao, ambao wamekataa majina yao yasitajwe, zimesema onyo hilo ni la mwisho.

Kwamba endapo wataendelea kujihusisha na vitendo hivyo, watasimamishwa masomo mara moja kulingana na kipengele 14(xi) wakati mashtaka dhidi yao yakiandaliwa na kushughulikiwa.

“Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umepata taarifa kuwa wewe ni miongoni mwa wanafunzi wanaojihusisha na vitendo kinyume cha sheria ndogo ndogo za wanafunzi wa Chuo Kikuu ya mwaka 2011, hususan makosa yaliyoainishwa kwenye vipengele 4.2(vxiii), 4.2(xix) na 4.2 (xxvi).

“Vitendo hivyo visivyokubalika ni pamoja na kupanga na kuhamasisha maandamano kinyume cha sheria, kujihusisha na vitendo vinavyokishushia hadhi chuo kwa kuanzisha kikundi/vikundi visivyoruhusiwa dhidi ya wanafunzi wenzako, Serikali na viongozi wa nchi.

“Kwa barua hii, unatakiwa kuacha mara moja vitendo hivi na endapo utakaidi, utakuwa umejiongezea makosa mengine kama yalivyoainishwa kwenye sheria ndogo ndogo za wanafunzi wa chuo vipengele vilivyotajwa,” ilieleza sehemu ya barua hizo.

Barua hizo zimetumwa nakala kwa Makamu Mkuu wa Chuo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utafiti), Mwanasheria Mkuu wa Chuo na Kaimu wa Baraza na Mkurugenzi wa Shahada za Awali kwa kumbukumbu.

Mmoja wa wanafunzi waliopewa barua hizo, alisema wamezichukua polisi Kituo cha Chuo Kikuu, baada ya kupigiwa simu Machi 14, mwaka huu wakitakiwa kuzichukua, lakini hawakuweza kwa sababu walikuwa wamefunga chuo.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles