24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA, SUMAYE WATINGA KISUTU, ULINZI WAIMARISHWA

Na Kulwa Mze, Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, wametinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi inayowakabili viongozi wakuu watano wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe.

Pamoja na Mbowe, viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo uchochezi, uasi na kuhamasisha maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Aquilina Akwilini.

Mbowe na viongozi hao wamefika mahakamani hapo saa moja na nusu kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana unaotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Aidha, mahakama hiyo leo ulinzi umeimarishwa ambapo polisi wamesheheni katika geti kuu la kuingia mahakamani na nje ya mahakama tangu saa kumi na moja alfajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles