24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mfalme amwambia Trump anataka suluhu ya kudumu

SAUDI ARABIA-UAE,

MFALME wa Saudi Arabia, Salman amemwambia Rais wa Marekani, Donald Trump katika mazungumzo ya  simu jana, taifa hilo  la kifalme lina nia  ya  kufikiwa  suluhisho la haki na la  kudumu  kuhusu mzozo wa  Palestina.

Mfalme Salman alisema  hilo,  ni sehemu kuu  ya kuanzia ya juhudi  za  pendekezo  la amani  la mataifa  za  kiarabu.

Viongozi  hao walizungumza kwa simu kutokana na  makubaliano ya kihistoria  yaliyosimamiwa na  Marekani  mwezi uliopita ambayo Umoja  wa Falme za Kiarabu  ulikubali  kuwa  taifa  la  tatu  la kiarabu  kurejesha  uhusiano  wa kawaida  na  Israel baada  ya Misri na  Jordan.

Mfalme Salman  alimwambia  Rais Trump anakubaliana  na  juhudi za nchi yake  kuunga  mkono  amani  na   Saudi Arabia inataka  kuona  suluhisho la kudumu  na  la  haki  katika  suala  hili  la Palestina chini  ya  juhudi  za  amani  za  mataifa  ya  kiarabu zilizopendekezwa  na  taifa  hilo  mwaka  2002.

Chini  ya pendekezo  hilo, mataifa  ya  kiarabu  yamependekeza kwa Israel  kurejesha  uhusiano wa  kawaida  ili  kufikiwa makubaliano ya kupatiwa  Wapalestina taifa lao  na Israel kujitoa kabisa  kutoka  katika  ardhi za mataifa  ya  kiarabu ilizoziteka  katika vita vya mwaka 1967 vya mashariki  ya  kati.

Saudi Arabia, mahali palipozaliwa uislamu  na maeneo  matakatifu, haiitambui Israel.

Hata hivyo, mwezi huu taifa  hilo  limesema  litaruhusu safari za  ndege  kati  ya  Umoja  wa  Falme  za  Kiarbu  na  Israel, ikiwa ni  pamoja  na  shirika  hilo  la  ndege la  Israel  kutumia  anga yake.

Mshauri  wa  Ikulu  ya  Marekani,  Jared Kushner alisema  ana  matumaini  mataifa  mengine  ya kiarabu  yatarejesha  uhusiano  wa  kawaida  na  Israel  katika muda  wa  miezi  michache.

Hakuna  taifa  lingine  la  kiarabu  lililosema  hadi  sasa   linatafakari  kufuata  mfano  wa  Umoja  wa  Falme za Kiarabu.

Mtoto mfalme Salman, mwana mfalme mteule Mohammed bin Salman na  Kushner walijadili haja  ya  Wapalestina na  Waisrael kurejea  majadiliano  na  kufikia  makubaliano  ya kudumu  ya  amani  baada  ya  Kushner kuzuru Umoja  wa  Falme  za Kiarabu mwezi  uliopita.

Makubaliano kati  ya  Umoja  wa  Falme za  Kiarabu  na  Israel yalipingwa kwa  kiasi  kikubwa  na  palestina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles