Mfahamu Shatti, msanii wa Kitanzania anayefanya vizuri Japan

0
1714

Nagoya, Japan

TANZANIA imebarikiwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji lukuki ambavyo kama vikitunzwa na kupewa nafasi vinaweza kuishangaza Dunia.

Miongoni mwa vijana hao ni Shatti, msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwasasa anaishi Japan huku akiendelea na sanaa yake chini ya usimamizi wa lebo ya Cutsleeve Records yenye asili ya Jamaica.
SHATTI NI NANI?

Ni msanii mahiri mwenye kipaji kikubwa ambacho ni nadra kutokea ambapo jina lake halisi ni Sameer Rashid Mrisho a.k.a Shatti aliyezaliwa Februari 12, 1999 jijini Dar es Salaam kwa wazazi Rashid Mrisho na Siaminah Kombakono.

ALIVYOANZA SANAA YA MUZIKI
Shatti, anasema alianza kupenda muziki akiwa mdogo kwa kusikiliza kazi za wasanii nguli duniani hivyo akajenga uwezo wake binafsi wa kufanya aina mbalimbali za muziki kama Dancehall na rap.
“Nilikiwa nasikiliza wasanii wakubwa kama Bob Marley, Peter Tosh, Michael Jackson, Tupac, Biggie na wengine ambao walinisaidia kukuza kipaji na uwezo wangu wa kufanya muziki,” amesema Shatti.

Uwezo wake unampa makali kama msanii ili ateme muziki mzuri ambai unafanya aorodheshwe kama Vybz Kartel au Mfalme Mpya asiye na ubishi wa Dancehall, mwimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo.

ALIVYOKWENDA JAPAN

Shatti aliondoka Tanzania kwenda Japan akiwa na miaka 21baada ya kusoma sekondari ya Benjamin William Mkapa iliyopo Dar Es Salaam, Tanzania ambapo alifaulu kwa kupata GED yake.

Msanii huyu sasa anajulikana kwa maelfu ya marafiki, familia ya muziki na mashabiki kama Shatti ambapo mwaka jana alipata umaarufu kama msanii anayekua haraka.

Kama msanii wa dancehall Shatti yupo tayari kuionyesha Dunia kile kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake.

AACHIA BLAZIN HOT

Meneja wa msanii huyo HIRO anasema unaweza kuendelea kumpa sapoti Shatti katika safari yake hii ya muziki ili azidi kufanya vizuri kwenye Dancehall, rap na Hip hop.
“Tumeachia ngoma mpya inaitwa BLAZIN HOT hivyo nahitaji sapoti ya mashabiki ili nizidi kufanya vizuri pia unaweza kutucheki kwenye Instagram kwa majina ya @Shatti_tz, @jdartmuzik na @cutsleeve_records,” amesema meneja HIRO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here