28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Messi atwaa Ballon d’Or ya sita

PARIS, UFARANSA

NAHODHA wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi, usiku wa kuamkia jana alitikisa dunia kwa kuandika historia mpya ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ya sita.


Tuzo hiyo inamfanya Messi kuwa mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo hiyo mara nyingi huku akifuatiwa na mpinzani wake Cristiano Ronaldo aliyechukua mara tano.


Tuzo hizo juzi zilitolewa huko nchini Ufaransa ambapo mastaa watatu Messi, Ronaldo na Van Dijk walikuwa wanawania, lakini Messi amefanikiwa kuibuka kinara huku akiwazidi wapinzani hao.


Wengi walimpa nafasi beki wa Liverpool, Van Dijk kutokana na mchango wake ndani ya kikosi hicho mwaka huu ikiwa aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku wakimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England.


Lakini Messi na yeye kwa upande wake alikuwa na mchango mkubwa kwa timu kuifikisha hatua ya juu, kama vile kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kuisaidia Argentina kufika fainali kwenye michuano ya Kombe la Copa America, lakini kura zimeamua Messi kutwaa tuzo hiyo.


Hata hivyo baada ya kutwaa tuzo hiyo, amewatoa wasiwasi mashabiki zake na kuwatisha wapinzani huku akisema bado yupo fiti na anauwezo wa kuchukua tena msimu unaofuata.


“Nitumie nafasi hii kuwashukuru waandishi wa habari ambao walinipigia kura. Nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha.


“Miaka kadhaa iliopita nilipata Ballon d’Or yangu ya kwanza mjini Paris, sikujua nini kitakuja kutokea kwa wakati huo, lakini sasa ninazo sita, hivi ni vipindi tofauti. Napenda niishukuru familia yangu na watoto wangu, mke wangu amekuwa akiniambia nisichoke kuwa na ndoto, kujituma, kubadilika, hivyo siwezi kuacha kumshukuru Mungu.


“Nina furaha kuandika historia hii binafsi pamoja na kwenye tasnia ya michezo, napambana kila siku kuwa bora nab ado nina nafasi nyingine ya kuwa bora na kutwaa tena tuzo hiyo msimu ujao bila ya kujali umri,” alisema mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles