22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Meridianbet Wawatembelea Sober House Kigamboni

Meridianbet kama ilivyo desturi na utamaduni wao wamekuwa wakijitahidi kushirikiana na jamii na kusaidia makundi yenye uhitaji na yanayokumbwa na changamoto mbalimbali.

Jana Meridianbet waliwatembelea waathirika wa madawa ya kulevya wanaopambana kuachana na matumizi ya madawa hayo chini ya taasisi ya Pillimissana Foundation huko Kigamboni.

Taasisi hiyo imeanzishwa takribani miaka kumi iliyopita, ikijishughulisha na watu wenye uraibu wa wa madawa ya kulevya, na kuwasaidia kupambana na hali hiyo.

Timu ya Meridianbet ilifika Sober House ya Pillimissana Foundation, Kigamboni na kupata mapokezi mazuri chini ya msimamizi wa kituo, ambaye alitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali, ikiwemo takwimu za wa waraibu waliofanikiwa kuhudumiwa ndani ya kituo hicho, pamoja na changamoto wanazo pambana nazo pale wanaporudi kwenye jamii.

Pia alieleza kituo hicho kimefanikiwa kutoa huduma kwa zaidi ya waraibu elfu mbili tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2012.

Timu ya Meridianbet ikiongozwa na Afisa Masoko wa taasisi hiyo Bwana Twaha Ibrahim, na balozi wa Kampuni hiyo bwana Jacob Mbuya walibainisha kuwa ni utaratibu wa Meridianbet kurejesha kwa Jamii, na wakati huu wameona wanaguswa na jitihada za Pillimissana Foundation na kuwaunga mkono katika jitihada hizo.

Timu ya Meridianbet iliunga mkono jitihada za Pillimissana Foundation kwa kutoa baadhi ya mahitaji ya msingi kama mchele, sukari, unga wa sembe na ngano, mafuta ya kupikia pamoja na Sabuni.

Meridianbet baada ya kukabidhi vitu hivyo kwa msimamizi wa kituo walipata wasaa wa kuonana na waraibu na kuzungumza nao maneno machache kuwatia moyo na kuwapongeza kwa kukubali kupata tiba ili kurejea katika hali zao za kawaida na kuongeza nguvu kazi ya taifa..

Pia mmoja wa waraibu, ambaye tumemhifadhi jina lake alipata nafasi ya kuzungumza na kuwawakilisha wenzake na kuishukuru sana timu ya Meridianbet kwa moyo waliouonesha na kuwataka wasiache kuendelea kurejesha kwa Jamii, kwani jambo zuri na la kuigwa.

Timu ya Meridianbet, inampongeza mratibu wa kituo hicho kwenye taasisi ya Pillimissana Foundation, Pilli Ramadhani Missana.  Ujumbe kutoka kituo hiki ni kuwa jamii inapaswa kutowatenga waraibu pale wanaporudi mitaani kwani inawavunja moyo na inaweza kuwa sababu ya kurejea kwenye utumizi wa madawa ya kulevya.

Meridianbet ambao ni mabingwa na wakongwe wa michezo ya kubahatisha kupitia tovuti na kasino ya mtandaoni, wakiwa na Jackpot kibao kupitia Meridianbet Casino, wamesisitiza kupitia afisa masoko wao Mr. Mohammed kuwa wataendelea kuwa karibu na jamii na kuwashika mkono wenye uhitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles