23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 287,512 kupatiwa chanjo ya Polio Songwe

Na Denice Sikonde, Songwe

Serikali mkoani Songwe imepanga ktoa chanjo ya polio kwa watoto 287,512 wenye umri chini ya miaka mitano katika kampeni itakayofanyika kwa siku Nne kuanzia Septemba Mosi hadi 4, mwaka huu.

Hayo amesema Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Cosmas Nshenye ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi katika kikao cha afya ya msingi ngazi ya mkoa kilichofanyika Agosti 30, na kujadili mikakati ya utekelezaji wa kampeni ya polio.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho.

Nshenye amesema kampeni hiyo ya polio watalamu watapita nyumba kwa nyumba na maeneo yote yenye watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya ili kufikia malengo ya kuwakinga watoto wote dhidi ya ugonjwa hatari wa polio.

Nshenye ametoa wito kwa wazazi/walezi wenye watoto wa umri chini ya miaka 5 kuhakikisha mtoto anapata chanjo ya matone ya Polio kwani Mtoto asiyepata chanjo Ni hatari kwa maisha yake na kwa jamii inayomzunguka.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani, Dk. Robert Hongo amesema kwa sasa Tanzania haina ugonjwa huo ila inachukua hatua usiingie nchini tangu utangazwe Januari 2022 nchini Malawi na Msumbuji ambazo ziko jirani na Tanzania na ukizingatia mwingiliano wa watu ni mkubwa hivyo hatua stahiki za kuwakinga watoto kwa chanjo ya matone ya polio ni muhimu.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amesema ni vyema jamii ikajua athari za ungonjwa polio kwa upana wake ili waweze kujitokeza kwa wingi kuwapatia chanjo watoto wao.

“Baada ya Nchi kutoa chanjo ugonjwa huu ulipotea sasa watu wengi wanausikia tu, ni vyema jamii ikapata athari za ugonjwaa huu kwa undani,” amesema Seneda.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Boniface Kasululu amesema katika Kampeni hii ya chanjo ya polio inayoanza Septemba Mosi mwaka huu watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano watapata chanjo hata kama ametoka kupata chanjo hiyo siku moja kabla.

Pia, Dk. Kasululu amesema ata kama Mtoto alipata chanjo ya matone kwa ratiba yake ya kliniki lakini ndani ya siku nne za kampeni hii Mtoto huyo atapata chanjo tena.

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Songwe, Moses Lyimo amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha kampeni inafanyika vizuri na kuwafikia watoto lengwa wote pamoja na kutoa elimu kwa wazazi/walezi kupitia vyombo vya Habari juu ya athari ya ugonjwa wa Polio kwenye jamii.

Kampeni hii ya polio ni ya nne tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu nchini Malawi lengo kuchukua hatua ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles