23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Medeama: Tunajua udhaifu wa Yanga

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Medeama ya Ghana wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Medeama ya Ghana wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam jana.

Na ADAM MKWEPU – DAR ES SALAAM

WAPINZANI  wa Yanga katika  michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Medeama, wametamba kujua udhaifu wa timu hiyo kwani wiki mbili walizotumia  kuwasoma wapinzani wao zinatosha  kuwapa pointi tatu  muhimu  kwenye mchezo wao unaotarajiwa  kuchezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itaingia dimbani ikiwa tayari imepoteza michezo miwili ya awali ya Kundi A, ukiwamo wa Mo Bejaia ya Algeria ilipofungwa bao 1-0 ugenini pia dhidi ya TP Mazembe, ilipofungwa bao 1-0 ikiwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kocha Mkuu wa Medeama, Prince Yaw  Owusu, alisema wachezaji wake watapambana  ili kupata pointi  tatu muhimu  zitakazowawezesha kuwa katika nafasi nzuri ya  kusonga  hatua inayofuata.

“Siwezi kusema moja kwa moja kwamba naijua Yanga au siijui, lakini muda niliotumia kuisoma utanisaidia kupata matokeo mazuri katika mchezo huo kwani nimeona udhaifu wao,” alisema Owusu.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Mohammed Tagoe, alisema kwa pointi moja waliyonayo haitoshi kujiamini na kudharau mchezo huo.

“Wengi wetu hatuifahamu vizuri Yanga, lakini haitoshi kusema mchezo huo utakuwa rahisi au mgumu kwani hata hii pointi moja tuliyonayo bado haitupi  hali ya kujiamini,” alisema Tagoe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles