27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenal yahofia kumkosa Alexis Sanchez

Alexis Sanchez
Alexis Sanchez

LONDON, ENGLAND           

KLABU ya Arsenal imeingia wasiwasi kumkosa mshambuliaji wao, Alexis Sanchez, katika michezo ya mwanzo ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

Mchezaji huyo hadi sasa bado hajaungana na wachezaji wenzake kwenye maandalizi ya msimu mpya kutokana na kusumbuliwa na enka.

Matatizo hayo aliyapata katika mchezo wa mwisho wa fainali ya Kombe la Copa America, huku timu yake ya taifa ya Chile ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wapinzani wao Argentina.

Mchezaji huyo alishindwa kuungana na timu hiyo ya taifa kwenye sherehe za ubingwa nchini Chile kutokana na kusumbuliwa na mguu huo, lakini alituma video yake kwa mashabiki akiwa nyumbani na kuwashukuru.

Hata hivyo, baada ya muda, kupitia akaunti yake ya Instagram, mchezaji huyo aliwatoa wasiwasi mashabiki wa Arsenal kwa kuwaambia kwamba anaendelea vizuri na baada ya muda atarudi uwanjani.

Lakini inadaiwa hali ya mchezaji huyo hadi sasa bado haijaimarika japokuwa yupo chini ya uangalizi wa madaktari.

Klabu ya Arsenal inatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya Liverpool, ambapo mchezo huo utapigwa Agosti 14 mwaka huu.

Hali ya mchezaji huyo inawapa maswali mengi wadau na mashabiki wa klabu hiyo, huku baadhi ya wachezaji kama vile Olivier Giroud, Mesut Ozil na Aaron Ramsey, wakiwa bado hawajajiunga na klabu hiyo hadi sasa.

Inadaiwa kwamba wapo kwenye mapumziko baada ya kuzitumikia timu zao kwenye michuano ya Kombe la Euro 2016, lakini klabu hiyo imeweka wazi kwamba wachezaji hao watajiunga Agosti 8.

Kutokuwepo kwa nyota wa klabu hiyo, Sanchez, Giroud na Welbeck, kunaweza kumpa nafasi kubwa Theo Walcott kuanza kwenye kikosi hicho, labda kocha Wenger afanye usajili wa mshambuliaji mpya wa kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles