Man Utd yaongoza kwa utajiri England

Manchester United

MANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester United, inaongoza kwa utajiri katika klabu za nchini England, huku thamani yake ikiwa imeongezeka kwa asilimia saba tofauti na msimu uliopita.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, klabu hiyo imeendelea kuongoza kwa utajiri ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.32, sawa na pauni bilioni 2.52.

Hata hivyo, hii ni kwa upande wa nchini England, lakini katika soka klabu ambayo inaongoza duniani kwa utajiri ni klabu ya Real Madrid, yenye thamani ya dola bilioni 3.65 sawa na pauni bilioni 2.77, ikifuatiwa na Barcelona yenye thamani ya dola bilioni 3.55 sawa na pauni bilioni 2.67.

Hata hivyo, klabu ya mchezo wa NFL ya nchini Marekani, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake duniani ikiwa ni dola bilioni 4 sawa na pauni bilioni 3.03. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi soka kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011.

Inadaiwa kwamba utajiri wa klabu ya Manchester United imezidi kuongezeka mara baada ya kusaini mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas, ambao ulikuwa na thamani ya pauni milioni 750.

Chakushangaza ni kwamba, Manchester United ina fedha nyingi lakini imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here