24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapaa viwango Fifa

FIFA RANKING

Na ADAM MKWEPU,

TANZANIA imepanda kwa nafasi 13 kutoka 136 hadi 123 katika viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), huku Argentina ikiendelea kuongoza ikifuatiwa na Ubelgiji.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda imeendelea kubaki nafasi za juu ambapo inashika nafasi ya 69 huku Kenya ikipanda kwa nafasi 43 kutoka nafasi ya 129 mwezi Mei hadi 86 na Rwanda iliyokuwa ikishika nafasi ya 103 imeshuka hadi nafasi ya 111.

Katika orodha iliyotolewa jana na Fifa, Algeria imeendelea kuwa vinara wa soka barani Afrika kwa kushika nafasi ya 32 duniani na kuishusha Ivory Coast iliyopo nafasi ya 35 ikifuatiwa na Ghana nafasi ya 36.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaongoza kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku ikishika nafasi ya 59 duniani na barani Afrika nafasi ya tisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles