23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MCT watoa pole vifo vya wanahabari TBC, watahadharisha

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM 

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limetoa salamu za pole kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayub Rioba, familia nzima ya televisheni hiyo na wafiwa wote kwa misiba ya wanahabari wake.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ilieleza kuwa Baraza lipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

Shirika hilo limepoteza wafanyakazi wake watatu katika kipindi cha wiki moja.

Hali kadhalika MCT ilitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa vyombo vya habari, wahariri na wanahabari wote kuzingatia mwongozo ulioutoa hivi karibuni kuhusu kujikinga dhidi ya virusi vya corona wakati wakiwa kazini na jinsi ya kuandika habari za janga hilo kwa weledi.

MCT pia imesisitiza kwamba janga limeishaingia chumbani hivyo ni vyema pale mwanahabari anaposikia habari zinazohusiana na maambukizi ya corona atoe taarifa kwa mhariri wake mara moja na achukue hatua za tahadhari ikiwamo kutokwenda kazini na kwenda hospitalini au kwenye kituo cha afya mara moja .

MCT pia imesisitiza viongozi wa vyombo vya habari kuchukua hatua za kuwalinda wafanyakazi wao wote kama inavyoelekezwa na watalaamu .

Wakati huo huo Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimewakumbusha wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kufuata miongozo ya kutekeleza majukumu yao kwa kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.

Tamwa imeshauri waandishi wa habari kutumia zaidi teknolojia ya mawasiliano  na imesisitiza kuwa wanahabari wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya kiutendaji kazi yatakayowaepusha dhidi ya virusi vya corona.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Rose Reuben imewataka wanahabari kuzingatia kuvaa barakoa (mask) hususani  wanapotekeleza majukumu yao kwenye vituo vya matibabu au karantini.

Pia imewataka kutoweka vifaa vyao vya kutendea kazi chini wakati wa kufanya kazi na kuhakikisha  wanavisafisha kikamilifu ili kuondoa maambukizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles