24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji Mkwawa kuliombea Taifa Januari Mosi

Na Asha Bani

Mchungaji wa Kanisa la Evangelical Brotherhood, usharika wa Mlima wa Moria, Emmanuel Mkwawa atafanya  kongamano maalum la  kuliombea taifa na viongozi Januari Mosi mwakani kwenye  viwanja vya Kanisa hilo, vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.

Mbali na maombi maalum kwa Taifa na viongozi pia kutakuwa na  uzinduzi wa Kitabu cha Elimu ya ndoto.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo  anatarajiwa kuwa mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki Dk.George Nangale .

Mchungaji Mkwawa  amesema hayo leo jijini Dar es Salamaa na kubainisha kuwa tayari watu kutoka mikoa mbalimbali nchini wameanza kuwasili jijini Dar es Dalaam kwa ajili ya ibada hiyo.

Aidha alitoa wito kwa watu wa dini zote kushiriki kwenye ibada hiyo ya kuliombea Taifa.

“Tumekuwa tukiliombea taifa mara kwa mara, hata Septemba mwaka huu tulifanya hivyo, lengo letu ni kuwa na taifa lenye upendo na amani wakati wote,” alisema Mchungaji Mkwawa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles