30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MBUNGE CUF ATAKA MAALIM SEIF AHOJIWE NA TAKUKURU

Na Elizabeth Hombo              |         


Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Ally amelitaka Bunge kuamuru, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kutopeleka hesabu za fedha za chama kukaguliwa na CAG.

Khatib alitoa kauli hiyo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2018/19.

“Hapa wote tumeng’ang’ania kwenye Sh trilioni 1.5 lakini mimi nataka zile Sh bilioni 200 zije Zanzibar. Leo nitakuwa tofauti kwa sababu nitapataje ujasiri wa kuhoji 1.5 trilioni wakati hesabu fedha za chama changu hazijapelekwa kwa CAG kukaguliwa?” amehoji.

Kutokana na hilo, amesema Katibu Mkuu wa Chama chake hajakitendea haki chama kwa kutopeleka mahesabu kwa CAG.

“Katibu Mkuu wangu ahojiwe na Takukuru kwanini hakupeleka hesabu za fedha zikaguliwe? Haya mambo yanataka ujasiri sana.

“Mheshimiwa Spika naomba kanuni inayomlinda mbunge inilinde maana isije ikaja kama ilivyowakuta wenzangu,” amesema.

Kutokana na hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemwmabia mbunge huyo kuwa katika jambo hilo wanamuunga mkono kwa kuwa ni la maana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles