26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

TUME YA UTUMISHI WA WALIMU YATENGEWA BIL.12

Na Mwandishin wetu     |      


Tume ya Utumishi wa Walimu imetengewa Sh bilioni 12 kwa mwaka wa fedha 2018/19, ambapo kati ya hizo Sh bilioni 7.8 ni za mishahara na Sh bilioni 4.6 ni za matumizi mengineyo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda wakati akijibu swali la Mbunge Singida Mjini, Mussa Sima.

Mbunge huyo alihoji Tamisemi haioni haja sasa ya kuziagiza rasmi Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwezesha Tume ya Utumishi ya Walimu kutekeleza baadhi ya majukumu yake ili walimu wapate huduma stahiki kwa wakati.

Akijibu swali hilo, Kakunda alisema: ” Katika mwaka wa fedha 2018/19 Bunge limeidhinishia tume hiyo fedha hizo ili ipate vitendea kazi kama magari, samani za ofisi na pia kugharamia vikao vya mashauri ya nidhamu na rufaa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles