26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mbunge Chumi afanya kongamano kumshukuru Rais Samia kwa kutatua changamoto

Na Raymond Minja, Mufindi

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi amefanya kongamano kubwa la kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka miradi ya Maendeleo jimboni humo.

Kongamano hilo limefanyika leo Juni 23,2022 ikiwa ni sehemu ya kupongeza miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa inayozunguka Mji wa Mfinga chini ya uongozi wa Rais Samia.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mbunge Chumi amesema jimbo la Mafinga Mjini ni kati ya yaliyopokea miradi mingi na mizuri, hivyo hawanabudi kumshukuru rais kwa miradi aliyowaletea.

Amesema moja ya changamoto iliyokuwa ikakabili jimbo hilo uhaba wa maji safi na salama lakini kwasasa linakwenda kuisha kabisa kwani wamepata mradi mkubwa wa maji na unaenda kumaliza kilio cha wananchi.

“Jamani nyie ni mashahidi tulikuwa na shida ya maji lakini sasa tumeshapata mradi mkubwa na ni kwa mara ya kwanza tunaenda kuchimbiwa visima vya maji na mabomba kutandikwa moja kwa moja bila ya kusubiri sijui kipindi kingine, sisi mradi unakwenda kukamilika moja kwa moja, nani kama mama…?,”amehoji Chumi.

Chumi amefafanua kuwa jambo lingine ambalo lilikuwa linawaumiza kichwa ni juu ya kupanda kwa gharama za mbolea lakini walipoenda bungeni wlijenga hoja na Serekali ikaamua kutoa VAT kwenye mbolea ili kumpunguzia mzigo mkulima.

“Kuna siku moja niko kwenye mkutano akaja mama mmoja na kunishika koti na kuniambia hebu niambiee baba, niuze debe ngapi za mahindi ili niweze kupata mbolea hata mfuko mmoja, lile jambo liliniuma sana ndio maana leo bei imepungua.

“Ngoja niwambie kitu ndugu zangu, unajua kazi ya mbunge sio kwenda kuizodoa Serekali bungeni bali ni kuchukua maoni na changamoto zinazogusa maisha ya watu wako na kwenda kujenga hoja bungeni ili kuweza kupata ufumbuzi na mwarobaini wa changamoto zao,” amesema Chumi.

Aidha ametajanjambo jingine kuwalilikuwa ni lile la serekali kutangaza kununua nguzo za umeme kutoka nje ya nchi na kuachana na zile zinazozalishwa hapa nchini jambo ambalo lilisababisha wafanyabiashara wa nguzo kuchanganyikiwa.

“Kwa Moyo wa dhati kabisa nimpongeze Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwa kusitisha zoezi la uagizaji nguzo kutoka nje yanchi kwani hatua hiyo lilikuwa likienda kuuwa uchumi wa watu wengi, hapa hatunabudi kumshukuru na kumpongeza Mama, lazima tusemee mama asante sana,” amesema Chumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mufindi, Daudi Yasini amesema wao kama watekelezaji wa Ilani ya chama wanajivunia Rais Samia kwani kwasasa wanaweza kutembea kifua mbele kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya.

Frida Kaaya ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi ambaye amempongeza mbunge Chumi kwa kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa wananchin wa jimbo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles