26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mmuya apongeza hatua ujenzi ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amepongeza maendeleo ya ujenzi wa ofisi  za  msajili wa vyama vya siasa  nchini zinazojengwa eneo la Kilimani jijini Dodoma zitakazogharimu  zaidi ya Sh bilioni 20.

Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Kaspar Mmuya (wa kwanza mbele) akiangalia  mpango kazi wa ujenzi wa  jengo la ofisi za Msajili wa vyama vya siasa Kilimani jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Juni 23, 2022 jijini Dodoma alipofanya ziara ya kutembelea  na  kukagua ujenzi huo unaofanywa na kampuni kutoka China ya Group Six International Limited ukisimamiwa na  mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Amesema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 akisisitiza kuongezwa kwa rasilimali watu, muda wa kazi pamoja na vifaa ili kufanya kazi ndani ya muda uliopangwa.

“Niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya Ofisi ya Msajili wa vyama vya sisisa  kwa usmamizi mkubwa mnaoufanya lakini endeleeni kuongeza umahiri na kuwasaidia wenzetu wa Group Six  International wafanye kwa matokeo zaidi,” amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Pia amemuagiza mshauri wa ujenzi kufika mara kwa mara katika eneo la mradi  na kufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine  kufahamu hali ya ujenzi na kutatua changamoto pindi zinapojitokeza kuhakikisha jengo linajengwa katika hali ya uimara, ubora na usalama.

“Nimshauri mtaalamu wetu awe anatembelea mara kwa mara jengo hili kujionea maendeleo ya kazi kama kuna shida yoyote inatatuliwa  kwa wakati na kufanya marekebisho yanayaotakiwa,”amesisitiza .

Aidha aliwahimiza kuongeza ubunifu wa utendaji kazi kwa kugawa maeneo na muda wa kukamilika kwa kazi kwani itasaidia kuhamasisha kazi kufanyika kwa mwamko na ubora zaidi kama njia ya kuendana na muda wa mkataba unavyotaka.

“Waongeze mtindo wa kufanya kazi kwa kupewa kipande cha kazi kwa muda inasaidia utendaji wa kazi na waangalie ubora usiathiriwe kwa sababu mtu anapopewa eneo lake na muda wa kikomo inamfanya ajitume kwa kasi kubwa,” ameeleza Mmuya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles