28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Mbunge ataka bodaboda iwe biashara rasmi

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

MBUNGE wa Lushoto, Shabani Shekilindi (CCM) amehoji ni kwanini Serikali haiwajengei uwezo wasafirishaji wanaotumia bobaboda ili iwe kazi rasmi yenye kutambulika kama kazi nyingine.

Akiuliza swali jana bungeni, Shekilindi alidai kwamba bodaboda ni kazi kama zilivyo kazi nyingine. “Je, Serikali haioni umuhimu wa kuirasimisha kazi hiyo ili iwe rasmi?” aliuliza.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde alisema Serikali imeweka mikakati ya kuwajengea uwezo waendesha bodaboda nchini ikiwemo kurasimisha kazi yao.

Mavunde alisema mipango iliyopo ni pamoja na kutoa mafunzo ya udereva kupitia Jeshi la Polisi kwa waendesha bodaboda na hatimaye kupatiwa leseni za udereva. Aidha, kama ilivyo vyombo vingine vinavyotoa huduma za usafiridhaji, usalama wa waendesha bodaboda na abiria umeendelea kusimamiwa na kulindwa wanapotekeleza majukumu yao barabarani.

Mipango ningine ni kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya waendesha bodaboda ili hatimaye viweze kuwezeshwa kwa mitaji na mafunzo kupitia mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na wadau wengine. Aidha, kuwapatia maeneo ya kuegesha bodaboda ya kuyatambua pamoja na kuwapatia vitambulisho.

Pia, kuwapatia waendesha bodaboda mafunzo ya ujasiriamali na hatimaye kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu na kuwaunganisha na taasisi nyingine zinazotoa mikopo. “Kuwapatia elimu juu ya faida za kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kuwaunganisha na mifuko husika,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles