28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa matumizi mabaya ya madaraka

NA AVELINE KITOMARY

DAR ES SALAAM

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru)  Mkoa wa Ilala imemfikisha mahakamani William Komba ambaye alikuwa Ofisa Utumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa makosa ya kutumia madaraka vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 na kuisababishia Serikali hasara.

Akizungumza na MTANZANIA jana Dar es Salaam, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava alidai kuwa Komba alitumia madaraka yake vibaya akiwa anatekeleza majukumu yake kwa kuingiza jina la Yotham Buratwaye kwenye mfumo wa Lawson Payroll kinyume na utaratibu na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 2.4.

Alisema mtuhumiwa amefikishwa mahakamani Februari 4, mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na dhamana ipo wazi na kesi hiyo itatajwa Februari 18, mwaka huu.

Wakati huo huo, mtaalamu wa mionzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Siriacus Mwombeki, amekamatwa na maofisa wa Takukuru kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa kinyume na sheria.

Myava alisema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makosa ya kushawishi, kuomba na kupokea rushwa ya Sh 500,000 kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.

Alidai kuwa Januari 28, mwaka huu, Mwombeki akiwa kwenye majukumu yake alishawishi, aliomba na kupokea Sh 40,000 ili aweze kumsaidia mtoto wa Kazembe Bundala (Nangale Kazembe) kufanyiwa upasuaji wa uvimbe kwenye goti.

Aliongeza kuwa tarehe hiyohiyo Mwombeki alishawishi na kuomba Sh 1,500,000 pamoja na mchele kilo kumi ili aweze kumsaidia mtoto wa Kazembe afanyiwe upasuaji wa goti.

Myava alidai kuwa Januari 31, mwaka huu, Mwombeki akiwa kwenye majukumu yake MOI alipokea Sh 500,000 kutoka kwa Bundala kama sehemu ya malipo ya fedha iliyoombwa ili kumsaidia mtoto wake kufanyiwa upasuaji wa goti.

Mtuhumiwa amefikishwa mahakamahi Februari 4, mwaka huu katika mahakama ya Wilaya ya Ilala na dhamana ipo wazi. Kesi itatajwa tena Februari 18, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles