31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mbosso kuzindua ‘Definition of Love’ Machi 20

Na Beatrice Kaiza, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Lebo ya Wasafi (WCB), Nasib Abdul “Diamond Platinumz” ametangaza tarehe ya uzinduzi wa Albamu ya Nyota wa bongo fleva Mbosso maarufu kama Mbosso Khan itakayofanyika ndani ya ukumbi wa Mlimani City, Machi 20, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 15, katika shughuli hiyo ya kutambulisha Albamu hiyo iliyobeba jina la “Definition of love”.
“Kwa mara ya kwanza Mbosso anazindua Albam yake yenye nyimbo 12 pamoja na nyimbo za ziada alizoshirikisha wanamuziki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nch,” amesema Diamond.

Aidha, Diamond amesema Mwaka huu anategemea kuwa na Shoo nyingi kutokana na mwaka jana kukumbwa na janga la virusi vya Covid 19.

“Mbosso alikua afanye shoo nyingi nje ya nchi ila kutokana na janga la Covid 19 ilibidi zisitishwe kutokana na sababu za kiusalama, hivyo kwa mwaka huu tutegemee Mbosso atapata nafasi ya kufanya shoo nyingi pamoja na ziara za mikoani,” amesema Diamond.

Kwa upande wake, Mbosso Khan, ameeleza sababu ya kutotumia lugha ya Kiswahili kwenye jina la Albamu hiyo kuwa ni kutokana na kuwa chachu ya kibiashara.

“Kama mnavyofahamu, hii ndiyo albam yangu ya kwanza, hivyo kutokana kwamba muziki wetu unaenda mbali kwa sasa ndio maana nimeamua kutumia kiingereza kwenye jina la albamu yangu ili kuleta chachu kwa mashabiki,” amesema Mbosso. Hata hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza katika Uzinduzi wa Albamu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles