22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Nyamagana yapata Mwenyekiti mpya

Na Sheila Katikula, Mwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Nyamagana mkoani Mwanza kimefanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya, Philipo Magoli, ambaye alifariki dunia mwaka jana.

Uchaguzi huo umefanyika leo Machi 15, katika ukumbi wa Chuo cha Banki Kuu kilichopo jijini hapa ukihusisha wagombea watatu ambao ni Boniphace Boniphace, Hassan Mambosasa na Kisali Simba.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athumani, alipokuwa akifungua kikao hicho amesema, kazi za vijana ni kujiamini, kujitambua na siyo kubeba mikoba ya wakubwa. Amesema wachague mtu Mwenye kujenga usawa, utendaji na ni muhimu kulinda jina lake na la chama.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Nyamagana, Malanyinyi Matukuta, amesema uchaguzi huo umeenda kwa haki na vijana ni waelewa na wanafanya kilichosahihi kuchagua kiongozi atakae kuwa bora kwa kutatua changamoto zinazowakabili.

Upande wake mshindi wa uchaguzi huo, Boniphace Boniphace aliyepata kura 247 kati ya 355, amesema ameahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa ushirikiano.

Aidha, mbali na Boniphace waliofuatia kwa kushika nafasi ya pili ni pamoja na Kisali Simba aliyepata kura 79 na Hussein Mambosasa kura 29.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles