26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kocha Simba: Ushindi nyumbani lazima

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema pointi tatu ni muhimu nyumbani dhidi ya Al Merrikh ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Gomes amesema Simba inahitaji alama 11 ili kujihakikishia nafasi ya kufika robo fainali kulingana na msimamo wa kundi ulivyo.

“Lazima tushinde, ni muhimu sana kupata alama tatu kesho kwa sababu kwenye kundi letu ili kufika robo fainali tunahitaji pointi 11. Kwa mazoezi tulifanya na kile nilichokiona, kikosi kipo vizuri,” amesema Gomes.

Aidha amesema katika mchezo huo atamkosa beki wake wa kati, Pascal Wawa, lakini ameandaa wengine kucheza nafasi yake kama vile Kennedy Juma na Erasto Nyoni.

Kwa upande wake, nahodha wa Simba, John Bocco, amesema wamejiandaa vizuri na wapo tayari kupigania pointi tatu katika mchezo huo licha ya kuwakosa mashabiki wao uwanjani ambao wamekuwa wakiwapa sapoti kubwa.

Simba ndiyo inayoongoza kundi A na pointi saba, kifuatiwa na AS Vita yenye alama nne sawa na Al Ahly, huku Al Merrikh ikiburuza mkia na pointi moja, timu zote zikicheza mechi tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles