26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania na Vatican kuhimiza amani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tanzania na Vatican zimeahidi kuendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kuhimiza amani, utulivu na usalama duniani.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, wakati alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski leo Machi 15, 2021 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Prof. Kabudi amesema mazungumzo yake na Askofu Mkuu Solczynski yalijikita zaidi kuhusu umuhimu wa Tanzania na Vatican kushirikiana katika mikutano ya Umoja wa Mataifa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika masuala mbalimbali yenye changamoto kwa binadamu.

“Tumeongelea umuhimu wa kulinda amani, utulivu na usalama duniani kote hasa katika maeneo yanayokumbwa na matatizo ya vita…….katika hilo pia tuliongela suala la amani na usalama katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika tukijua kuwa kuna maeneo yanayohitaji amani ikiwemo eneo la kaskazini mwa Masumbiji, na mashariki ya Demokrasia ya Kongo,” amesema Pro. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni na hata sasa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji mshikamano wa mataifa yote duniani ili kuweza kuyakabili hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu amani, utulivu, majanga, na magonjwa ya mlipuko kama vile Covid 19, na yale yanayohusu umasikini na hali yamaisha ya watu kubaguliwa na kuonewa.

“Mfano katika mapambano dhidi ya Uviko 19, Vatican na Baba Mtakatifu wanayo nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika eneo hilo katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya Covid 19 hayageuzwi kuwa katika masuala ya kibiashara na kisiasa na badala yake mapambano hayo yazingatie utu, undugu na imani, ameongeza Pro. Kabudi

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika MAshariki, William Tate Ole Nasha akiongea na Balozi wa Algeria
nchini, Ahmed Djellal wakati walipokutana kwa mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski, amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya haki, utu, amani na utulivu.

“Maongezi yangu na Waziri yalikuwa mazuri kwani tuliongelea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa binadamu yakiwemo masuala ya kukuza diplomasia yetu pamoja na masuala ya amani na usalama duniani,” amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Katika tukio jingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Tate Olenasha amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria hapa nchini, Ahmed Djellal, ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha diplomasia baina ya Tanzania na Algeria. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles