28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tuzo za Grammy: Burna Boy na Wizkid washinda tuzo za Grammy

Wasanii maarufu wa Nigeria Burna Boy na Wizkid wameshinda tuzo za Grammy za mwaka huu wa 2021.

Burna Boy ameshinda tuzo ya kipengele cha Albamu bora ya muziki wakati Wizkid ameshinda katika video bora zaidi kwa wimbo wake aliomshirikisha Beyoncé unaoitwa Brown Skin Girl, kutoka Lion King: Albamu ya The Gift.

Binti yake Beyoncé Blue Ivy alikuwa mshindi katika wimbo huo huo. Katika kipengele cha video bora, tuzo inatolewa kwa msanii, muongozaji wa video na muandaaji wa video pia.

Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, ambaye ameshiriki kwa mwaka wa pili ameshinda katika albamu yake ya Twice As Tall .

Tuzo ya Grammy ya 63 imefanyika mjini Los Angeles. Kwa kawaida huwa sherehe kubwa ya muziki huwa inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na janga la corona.

Hakuna watazamaji, na watumbuizaji walikuwa wametengwa katika majukwaa matano, na wakiwa kwa umbali. Burna Boy(29), amewashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian, Tinariwen.

Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, ambaye ameshiriki kwa mwaka wa pili ameshinda katika albamu yake ya Twice As Tall .

Wizkid

Tuzo ya Grammy ya 63 imefanyika mjini Los Angeles. Kwa kawaida huwa sherehe kubwa ya muziki huwa inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na janga la corona. Hakuna watazamaji, na watumbuizaji walikuwa wametengwa katika majukwaa matano, na wakiwa kwa umbali. Burna Boy, mwenye miaka 29, amewashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian, Tinariwen.

Burna Boy amechaguliwa katika kipengele kilekile cha mwaka 2019 – kinachojulikana kama ‘Best World Music Album’ – lakini Angelique Kidjo aishinda katika tuzo za mwaka 2020.

Ingawa Kidjo aliamua kutoa ushindi wake kwa Burna Boy, alisema: “Burna Boy ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanatoka Afrika ambao wanabadili mtazamo wa muziki wa Afrika.”

Mwanamuziki huyu aliyezaliwa Nigeria, Burna Boy alizindua albamu yake ya kwanza ya LIFE, mwaka 2013. Na baadae alizindua albamu ya Redemption mwaka 2015 na Outside mwaka 2018 ambayo ilijumuisha ngoma iliyovuma kimataifa ya , Ye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles