24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Habari njema kwa Wananchi wa Kinyerezi, Mongo la Ndege na Kifuru

Na Crispin Gerald, DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekamilisha zoezi la kuunganisha bomba kubwa la inchi 10 maeneo ya daraja la kinyerezi litakalopokea maji kutoka kwenye mradi mkubwa wa maji wa Pugu-Gongo la mboto kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kinyerezi, Mongo la ndege, Kifuru na Vindini.

Zoezi la kuunganisha bomba ni sehemu ya kazi inayoendelea ya kujenga mtandao wa kupokea maji kutoka kwenye tanki la Maji Pugu na utakaohudumia wakazi takribani 1,000 wa maeneo hayo.

Akizungumzia zoezi hilo Meneja wa Usambazaji Mhandisi Tyson Mkindi amesema kazi iliyofanyika ni kubadilisha mtandao wa maji uliokuwepo kwa kuweka bomba lipya la inchi 10 litakaloweza kupokea na kusambaza maji.

“Kazi imekamilika na baada ya kukamilisha kujenga mtandao tutaruhusu maji yaweze kufika kwa wananchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles