28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kelvin Chale ashinda uchaguzi wa Mwenyekiti UVCCM Songea Mjini

Na Mwandishi Wetu, Songea

Kelvin Chale amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Wilaya (UVCCM), Songea mjini baada ya kuwabwaga wenzake kwa kura 185.

Uchaguzi huo umefanyika leo Machi 15, 2021 ukumbi wa Open University Manispaa ya Songea kwa lengo la kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti Wilaya baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Issa Chiwaneke kushinda Udiwani kata ya Ndilima Litembo.

Kelvin Chale Mshindi wa nafsi ya Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Songea mjini akiwashukuru wajumbe baada kumpa ushindi wa kishindo na kutangazwa kuwa mshindi

Akitangaza Matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mwanahamisi Manyopo, amemtangaza Mshindi kuwa ni Kelvin Chale (185) akifuatiwa na Kalela Khalifa (130), Renatus Chale (32) na Rustika Komba (1).

Aidha amesema wajumbe waliopiga kura ni 354 ambapo kura halali zilikuwa 348 na ziliozoharibika 6.

Kwa upande wake Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti, Kelvin Chale, amesema atahakikisha anawapigania vijana kupata mkopo asilimia 4 toka mwenye Halmashauri iliziwasaidie kuanzisha biashara ndogondogo .

Aidha, ameahidi kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na viongozi wenzie ili mikopo watakayopata iwe na manufaa kuinua uchumi wa vijana wenzie,ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha pamoja kwani Jumuiya hiyo kwa sasa imegawanyika na kwamba yeye atawaunganisha pamoja na kuwaletea maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles