25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

MBEYA CITY: HATUTAMWACHA MTU SALAMA SOKOINE

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Mbeya City umesema utahakikisha unavuna pointi tisa katika michezo yake mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa  Sokoine jijini Mbeya.

Ratiba ya Ligi Kuu inaonyesha kuwa timu hiyo itacheza michezo yake mitatu mfululizo kwenye Uwanja wa Sokoine, ilianza kwa kuivaa Majimaji na kushinda mabao 2-0.

Timu hiyo itashuka tena dimbani Jumapili kuumana na Ndanda FC, kabla ya wiki ijayo kuikabili Njombe Mji.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja, alisema timu hiyo imeweka mikakati ya kutumia vema faida ya kucheza nyumbani kwa kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye michezo yake yote.

“Tumepata bahati ya kucheza michezo mitatu mfululizo nyumbani, hivyo tumeweka mikakati imara ya kuhakikisha tunatumia vizuri fursa hiyo kwa kukusanya pointi zote.

“Tunataka kuendeleza wimbi la ushindi tuliloanza nalo katika mchezo wa kwanza, tumejiandaa vizuri kubakiza pointi tatu nyingine Jumapili dhidi ya Ndanda FC, hilo linawezekana kwa kuwa tunaungwa mkono na mashabiki wetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,694FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles