30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

MOURINHO: NEYMAR ANGEPANDISHA DAU LA LUKAKU

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, anaamini kuwa uhamisho wa Romelu Lukaku kujiunga na timu hiyo ungekuwa mgumu sana endapo Neymar angekuwa wa kwanza kusajiliwa na PSG.

Kocha huyo anaamini alifanya maamuzi sahihi ya kumsajili mchezaji Lukaku kutoka Everton kabla ya siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa kuwa thamani yake ingekuwa kubwa zaidi.

Mourinho alimsajili mshambuliaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 75 ambazo ni zaidi ya bilioni 215 za Kitanzania, wakati huo Neymar akivunja rekodi ya usajili kwa uhamisho wa pauni milioni 198 zaidi ya bilioni 569, kutoka Barcelona kujiunga PSG.

Kocha huyo amedai endapo Neymar angekuwa wa kwanza kuhama kabla ya Lukaku basi dau la Lukaku lingezidi kuwa kubwa na ingewapa wakati mgumu wa kumsajili mshambuliaji huyo raia wa nchini Ubelgiji.

“Naweza kusema sisi Manchester United tuna akili sana, tulikuwa na imani kwamba kuna uwezekano mkubwa wa soko kubadilika kama tungeshindwa kusajili mapema kabla ya uhamisho wa Neymar.

“Tulikuwa tunajua kwamba, Neymar anaweza kuondoka kwa uhamisho wa kiasi kikubwa cha fedha, hivyo tulilazimika kufanya usajili wa mapema ili kuupisha usajili huo mkubwa.

“Mawakala wengi wangepandisha ada ya uhamisho wa wachezaji wao kutokana na Neymar kuondoka kwa kiasi kikubwa na tunaamini thamani ya Lukaku ingekuwa mara mbili ya ile ambayo tumemsajili, hivyo uhamisho wake ungekuwa mgumu sana,” alisema Mourinho.

Kocha huyo katika kipindi hiki cha majira ya joto alifanya usajili wa Nemanja Matic kutoka Chelsea kwa pauni milioni 40, Victor Lindelof kutoka Benfica kwa pauni milioni 30.7 pamoja na Lukaku kwa pauni milioni 75.

“Nadhani Lukaku ningemsajili Agosti 31, bei yake ingefikia pauni milioni 150, Matic angefika pauni milioni 60, hadi 70, hatua hiyo ingefikia kutokana na uhamisho wa Neymar kubadilisha soko la wachezaji,” aliongeza Mourinho.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchester United, inasema kwamba uongozi wa timu hiyo upo kwenye mipango ya kutaka kumwongezea mkataba mpya kocha huyo ili aendelee kuwa hapo kwa muda mrefu na kuwapa mataji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles